Jumatatu 6 Oktoba 2025 - 15:56
Wanaharakati wa Flotilla ya “Ṣumūd‌” Wafichua Uhalifu uliofanywa na Wavamizi wa Kizayuni

Hawza/ Wanaharakati waliokuwa washiriki katika Flotilla ya Kimataifa ya Ṣumūd‌ walisema: “Katika vizimba vilizotengenezwa kwa ajili ya watu watano, waliwekwa watu kumi na tano. Tuliona maandiko yaliyokuwa yameandikwa kwa damu kwenye kuta. Tulisoma majina ya watoto yaliyokuwa yameandikwa na mama zao kwenye kuta. Tuliweza kuelewa kwa kiasi kidogo tu mateso wanayoyapitia Wapalestina. Hawakutupa maji; walituambia tunywe maji ya chooni. Tulikaa na njaa kwa saa takriban 40.”

Kwa mujibu wa taarifa ya Kitengo cha Habari za Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, watu 137 waliokuwa washiriki wa Flotilla ya Kimataifa ya Ṣumūd‌ — wakiwemo raia 36 wa Uturuki na raia 23 wa Malaysia — waliwasili mjini Istanbul baada ya kuachiwa kutoka kwenye vifungo vya utawala wa Kizayuni.
Wanaharakati hawa, ambao walikuwa wameelekea maji ya kimataifa kuvunja mzingiro wa Ghaza, walizungumza na wanahabari wakielezea kwa undani mashambulizi yanayofanywa na Israel dhidi ya meli na mienendo isiyo ya kibinadamu ya wanajeshi wa utawala huo.

Mwandishi wa habari wa Kituruki, Ersan Çelik, ambaye alikuwa sehemu ya msafara huo, alisema:

“Israel ilitufanyia ukatili mkubwa na kwa njia isiyo ya ubinadamu. Tuliteswa kimwili na kisaikolojia. Baadhi ya marafiki zetu walijeruhiwa. Hawakutupa maji wala chakula, hata walitaka tule mabaki ya chakula chao, jambo ambalo tulilikataa. Hatimaye, kwa juhudi za serikali ya Uturuki, tuliweza kurudi. Tumefanikiwa kujikwambua kwenye vikwazo kwa sababu hali ya kisaikolojia ya Wazayuni imeporomoka sana; hawajui wafanye nini. Sasa dunia nzima inawachukia.”

Çelik akaongeza kusema: “Mbele ya macho yetu, Greta Thunberg, mwanaharakati wa mazingira kutoka Sweden, aliteswa kikatili. Ni msichana mdogo. Walimlazimisha abusu bendera ya Israel — jambo lile lile walilofanya Wanazi.”

Mwanaharakati wa Kituruki Dashkaran naye alisema kuwa bado kuna idadi ya wanaharakati walioko kizuizini nchini Israel, na akaongeza kuwa:

“Ubalozi wetu umetupa ahadi ya kuwarudisha. Tumefanikiwa kuvunja mzingiro na kuionesha dunia kiwango cha ukatili wa Israel. Hili ndilo lilikuwa ndio lengo letu — na tumelifanikisha.”

Muhammad Amin Yıldırım, Rais wa Siyer Foundation na mmoja wa washiriki wa Flotilla ya Ṣumūd‌, alisema lengo lao lilikuwa ni kuamsha uelewa wa dunia kuhusu mauaji ya halaiki yanayoendelea Ghaza.

“Meli zetu zilizingirwa kisha tukakabiliwa na udhalilishwaji mkubwa. Sasa tunaelewa vizuri zaidi yale ambayo Wapalestina wamekuwa wakipitia kwa miaka mingi. Hata maji ya kawaida ya kunywa hatukupewa; tulinyimwa maji na ibada kwa siku tatu kamili. Mwenendo wao ulikuwa sawa na jinai walizokuwa wakizifanya daima.”

Ekbal Gürpınar naye alisema: “Wavamizi tena mara nyingine wameonesha udhaifu na sura yao ya kweli mbele ya mitazamo ya dunia. Nilikuwa katika kizimba kimoja na mbunge kutoka Italia. Usiku mmoja walituhamisha vyumba mara kadhaa, na walitutisha kwa sauti za kinyama. Askari wanawake walikuwa wakatili zaidi kuliko wanaume. Walitudhihaki, kututesa kwa njaa, kuchukua dawa zetu na kuiba mali zetu. Askari waliweka kompyuta na simu zetu kwenye mifuko yao. Asili ya uwepo wao ni uporaji — kama walivyoiba ardhi ya Wapalestina.”

Gürpınar alisisitiza: “Israel imefikia ukingoni, mataifa yote sasa yanawachukia. Mbunge wa Italia aliwaambia wazi: ‘Ninyi ni wasaliti. Zamani tuliwatetea, lakini sasa nitaufichua uso wenu wa kweli duniani.’ Wote tumedhamiria kurudi na kutoa taarifa dhidi ya Israel.”

Mwanaharakati mwingine, Ayçin Cantoğlu, alisema: “Wakati wa kukamatwa, baadhi ya maafisa walizungumza nasi kwa Kituruki. Mmoja aliniuliza umetoka wapi, nikasema kutoka Muğla. Akasema: ‘Unajua uko wapi? Uko Israel. Ghaza haipo tena.’ Nilimtazama na nikacheka kwa dhihaka.”

Akaongeza kuwa usiku huo huo, Itamar Ben-Gvir, Waziri wa Usalama wa Ndani wa utawala wa Kizayuni, alifika kwa ajili ya ‘ukaguzi’: 

“Walituhifadhi kama wanyama ndani ya chumba kama ngome. Ben-Gvir aliwasili na wanahabari na kusema: ‘Hawa hawawahurumii watoto wa Quds.’ Tulijibu kwa kelele: ‘Funga mdomo wako, ewe mhalifu wa mauaji ya halaiki!’ Baada ya hapo mazingira ya gereza yakawa magumu zaidi, lakini hatujutii. Tulifanya jambo sahihi. Katika vizimba vilizotengenezwa kwa ajili ya watu watano, waliwabana watu kumi na tano. Tuliona maandiko kwa damu kwenye kuta. Tulisoma majina ya watoto yaliyokuwa yameandikwa na mama zao. Tuliweza kuhisi kwa sehemu ndogo mateso ya Wapalestina. Hawakutupa maji, walituambia tunywe maji ya chooni. Tulikaa njaa kwa saa 40.”

Alipoulizwa kuhusu jitihada za askari wa Israel kuwavua hijabu wanawake, alisema:

“Walifanya upekuzi mara kwa mara katika kila kituo. Hata ndani ya midomo na katikati ya meno yetu walichunguza. Walituita ‘magaidi,’ lakini tulipowatazama machoni tuliwaambia: ‘Sisi si wakosaji; ninyi ndio mliovunja sheria na kututeka.’ Ikiwa lengo lao lilikuwa kutuvunja moyo, hawakufanikiwa. Tulibakia tukipaza kauli zetu hadi dakika ya mwisho na tukalijaza gereza lao kwa sauti zetu za kupinga.

“Muhammad Jamal,” mwanaharakati kutoka Kuwait, alisema: “Katika operesheni ya kukamatwa, takribani askari maalum 700 wa Israel walihusika. Saa kumi na mbili alfajiri, askari ishirini walilitwaa jahazi letu. Walitushikilia chini ya jua kwa saa 12 bila chakula, wakitupa ruhusa ya kunywa maji pekee. Katika bandari ya Ashdod, pia polisi walitufanyia vitendo vya udhalilishaji.”

Tommaso Bortolazzi, nahodha wa Kiitaliano wa meli Maria Cristina, aliongeza kusema: “Nilijiunga na msafara wa Ṣumūd kwa sababu sikuweza kuyafumbia macho mauaji ya kimbari. Siku za mwisho gerezani zilikuwa ngumu sana. Marafiki zangu Waturuki wote walikuwa Waislamu. Walipokuwa wakisali, polisi wa Kizayuni waliwazuia. Kwa kujibu, mimi pia nilitamka Shahada na nikasilimu; nilihisi kama nimezaliwa upya. Natumaini mataifa huru na ya kidemokrasia duniani yatajiunga na mapambano haya dhidi ya Israel, kwani wakati wa kukomesha mauaji haya ya kimbari umefika.”

Semenur Sönmez Yaman, naibu mkuu wa mawasiliano wa Shirika la Wanawake na Demokrasia (KADEM), alisema: “Israel haikuacha kutumia mbinu yoyote kutudhalilisha. Walitushikilia katika joto na baridi kali, lakini kitendo kibaya zaidi kilikuwa kunyang’anywa hijabu zetu.”
Akiwa ameinua fulana aliyokuwa ameivaa kichwani kuelekea kwenye kamera, alisema:
“Hii fulana niliyo nayo kichwani sasa ndiyo mbadala wa ushungi wangu. Kwa kisingizio cha uchunguzi wa kiafya, walituvua nguo na kwa makusudi wakachukua shungi zetu licha ya upinzani na malalamiko yetu. Wanawake wasio na hijabu waliokuwa pamoja nasi walitupa fulana zao ili tuweze kufunika vichwa vyetu.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha